Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 23 April 2024

DKT. NCHEMBA ATETA NA MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA DUNIA KUNDI LA AFRIKA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania.

Na Joseph Mahumi, WF, Washington.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) jijini Washington D.C, Nchini Marekani, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Benki hiyo na Tanzania.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko (hayupo pichani) Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Ujumbe wa Tanzania (kushoto) ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ukiwa katika kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko (katikati), akizungumza wakati wa kikao na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), kilichofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Washington D.C, nchini Marekani. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji Mbadala wa Benki ya Dunia, anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency (AfG1), Dkt. Zarau Kibwe (kushoto), Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Venuste Ndikumwenayo (kulia).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko (wa tatu kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tatu kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji Mbadala wa Benki ya Dunia, anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency (AfG1), Dkt. Zarau Kibwe (wa kwanza kulia), Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Venuste Ndikumwenayo (wa pili kushoto) na Afisa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Charles Longo (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika Makao Makuu ya Benki ya Dunia, jijini Washington D.C, nchini Marekani.

BIMA YA AFYAPASS KUTOKA VODABIMA YARAHISISHA HUDUMA ZA AFYA

Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dk. Baghayo Saqware (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Assemble Insurance, Tabia Massudi (kushoto) wakiwa na vipeperushi kuashiria uzinduzi wa kampeni ya “VodaBima kidigitali, Ni Chap, ni Nafuu” inayohamasisha matumizi ya Bima Kidigitali uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia huduma zake za VODABIMA zinazopatikana kwa M-Pesa, itanufaisha wagonjwa wa kulazwa na kutwa, vyombo vya moto na bima ya maisha kwa mtu mmoja mmoja na vikundi kwa gharama nafuu.

Mwamko mdogo wa Watanzania kuhusu bima ya afya ni mojawapo ya changamoto katika kutoa huduma bora za afya kwa wote kutokana na idadi ndogo ya Watanzania wenye bima. Takwimu za Wizara ya Afya (2022) zinaonesha kuwa asilimia 15 tu ya Watanzania, sawa na watu milioni 9.1, walikuwa na bima ya afya mwishoni mwa mwaka 2021, ikishuka kutoka asilimia 32% mwaka 2018.

Vodacom Tanzania PLC imeungana na Assemble Insurance na kuja na bima ya afya ya kijiditali kupitia simu ya mkononi iitwayo AfyaPass ambayo ni rahisi, nafuu, na inapatikana kwa Mtanzania popote pale alipo
nchini. Bima hii inapatikana kwa bei nafuu ya Shilingi 70,000 kwa mwaka kwa mtu mmoja na vifurushi vya familia kutoka TZS 105,000 kwa watu wawili hadi TZS 385,000 kwa watu sita kwa mwaka na inapokelewa katika hospitali binafsi na za serikali. Kwa malipo kidogo ya nyongeza, mtumiaji anaweza kupata huduma za uzazi, radiolojia, mazoezi tib ana nyingine nyingi.


Unaweza kujiunga na AfyaPass kupitia M-Pesa ikiwa ni moja ya aina za bima zinazotolewa kupitia VodaBima yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za bima kwa kila mtu bila kujali kipato chake au umbali wa eneo anapotoka nchini Tanzania.

VODACOM YATOA MSAADA KWA WAHANGA WA MAFURIKO PWANI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge (wa pili kulia) akipokea msaada wa kibinadamu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko ya Rufiji na Kibiti wenye thamani ya takribani shilingi milioni 250 uliotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation. Msaada huo ulikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Vyombo vya Habari wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Annette Kanora (katikati). Wengine pichani kutoka kushoto ni Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald na Meneja Mauzo wa eneo hilo, Suleiman Amri na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele (kulia). Msaada huo ulikabidhiwa mwishoni mwa wiki mjini Kibiti.

ADVANCING CIRCULARITY WITH THE GALAXY S24 SERIES

  • Samsung is celebrating Earth Day by reflecting on the Galaxy S24 series and spotlighting the work of young changemakers
Samsung is on a journey to harness the power of technology to open more possibilities for people and the planet. To celebrate Earth Day, Samsung would like to reflect on how we’re advancing our mission and creating a more sustainable future — whether we’re increasing the use of recycled materials in our Galaxy mobile devices or collaborating with the United Nations Development Programme (UNDP).

Finding the Balance Between Innovation and the Environment

Samsung is reimagining how Galaxy technology is designed and packaged to do more with less when it comes to our planet’s natural resources. For the last decade, we have worked to innovate high-performance components that are made with recycled materials.

We took an important step in 2022 when we incorporated recycled discarded fishing nets, also known as ghost nets, in the Galaxy S22 series. Recycled materials can now be found in all Galaxy mobile products, including smartphones, tablets, PCs and wearables. At the same time, we have expanded our use to a greater variety of materials, from several different types of plastics to metals and glass.

The Galaxy S24 series takes these actions one step further. For the first time in any Galaxy device, we developed key device components with recycled cobalt, rare earth elements and steel. The battery in the Galaxy S24 Ultra contains a minimum of 50% recycled cobalt, and 100% recycled rare earth elements and a minimum of 40% recycled steel were used in the speakers.

Samsung has a long history of addressing the pervasive challenge of plastic waste through our recycled material innovations, and recycled plastics continue to play an important role in the Galaxy S24 series. The Galaxy S24 series maintains our use of recycled plastics sourced from discarded fishing nets, water barrels and PET bottles.

NMB YADHAMINI MKUTANO MKUU ALAT TAIFA; RAIS SAMIA KUFUNGUA LEO

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 120, Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Sima Constantine Sima (katikati) kwa ajili ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa utakaofanyika kuanzia leo jijini Zanzibar. Kushoto ni Afisa Mkuu Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Alfred Shao, Kulia ni Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame (kulia) na Kaimu Katibu Mkuu wa ALAT Taifa, Mohammed Maje (wa pili kulia).

Benki ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. Mil. 120 kudhamini Mkutano Mkuu wa 38 wa Mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT Taifa), unaofunguliwa Jumanne Aprili 23 na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ukiwakutanisha washiriki zaidi ya 600.


Kiasi hicho kinachodhamini mkutano wa mwaka huu unaofanyika chini ya kaulimbiu; ‘Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Jambo Letu; Shiriki kwa Maendeleo ya Taifa,’ kinafanya udhamini wa NMB kwa ALAT Taifa kufikia Sh. Bil. 1.2 katika kipindi cha miaka nane.


Mkutano Mkuu wa ALAT, unaowapa fursa viongozi wa Serikali Kuu kutoa Maelekezo na Miongozo ya Kisera kwa Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, wakiwemo Mameya wa Majiji na Manispaa, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmshauri 184 (za Tanzania Bara), utafungwa Aprili 25 na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.


Kwa miaka nane sasa, NMB na ALAT zimekuwa na ushirikiano endelevu katika masuala mbalimbali kwa maendeleo ya Halmashauri zote nchini, ikiwemo kudhamini na kufanikisha vikao na Mikutano Mikuu ya Mwaka ya ALAT, ambayo kimsingi ndio chachu ya utendaji bora kwa Halmashauri hizo.


Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, iliyofanyika Golden Tulip Zanzibar Airport Hotel, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna, alisema wanajivunia kuwa wabia wakubwa wa ALAT, na kwamba wanathamini heshima ya kipekee wanayopewa na uongozi wa jumuiya hiyo.

Monday 22 April 2024

USIKOSE EVERTON vs LIVERPOOL NDANI YA DStv COMPACT


Piga *150*53# kulipia kifurushi chako mapema

#mfalmewasokanidstv
#mfalmewabomanidstv
#unakosaje

TANZANIA YAISHAURI BENKI YA DUNIA KUWEKA VIPAUMBELE MIRADI YA MAENDELEO AFRIKA

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (katikati), akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Benki ya Dunia) (WBG Africa Group 1 Constituency) uliofanyika Washington DC, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini humo, ambapo alitumia fursa hio kuiomba Benki ya Dunia kutilia maanani vipaumbele vya maendeleo vya nchi za Afrika ikiwemo kuzipatia fedha na ujuzi ili ziweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (katikati) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (kulia), wakifuatilia Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Benki ya Dunia) (WBG Africa Group 1 Constituency), wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, Nchini Marekani.
Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Benki ya Dunia) (WBG Africa Group 1 Constituency) ukiendelea, mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yenye kauli mbiu ya “Vision to Impact” inayoendelea jijini Washington D.C, Nchini Marekani.

Na Scola Malinga, WF, Washington.

TANZANIA imeishauri Benki ya Dunia kutilia maanani vipaumbele vya maendeleo vya nchi za Afrika ikiwemo kuzipatia fedha na ujuzi ili ziweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Benki ya Dunia) (WBG Africa Group 1 Constituency) uliofanyika Washington DC, nchini Marekani.

Alisema kuwa Benki ya Dunia imekuwa inasaidia kwa kiasi kikubwa nchi za Afrika na sasa wasaidie kuwekeza nguvu zaidi kwenye miradi ya Maendeleo ili kuinua uchumi kwa haraka.

“Tunaiomba Benki ya Dunia inapopitia matarajio yao iweke kipaumbele kwa Afrika na kwa nchi moja moja na kutoa nyongeza ya rasilimali fedha,” alisema Dkt. Mwamba.

TOSHIBA RECEIVES ORDER FOR POWER GENERATION EQUIPMENT FOR RENOVATION OF GEOTHERMAL POWER PLANT IN KENYA

  • Toshiba’s high-performance turbines and generators have improved power generation output by 40% compared to conventional models
NAIROBI. Toshiba Energy Systems & Solutions Corporation (Toshiba ESS) announced today that it has received an order from SEPCOIII Electric Power Construction Co., Ltd. for steam turbines and generators for the geothermal power plant equipment renovation of Units 1 through 3 at the old 45MW Olkaria I geothermal power plant in Kenya. The steam turbines and generators will be shipped to the site by December 2025.

Olkaria I geothermal power plant is the oldest geothermal power plant in Kenya and has been in commercial operation by the Kenya Electricity Generating Company PLC (hereinafter “KenGen”) since 1981.

Units 1 through 3 of the plant need renovation due to aging, and Toshiba ESS’s steam turbines and generators have been selected for the renovation. This will increase the power output of Units 1 through 3 from the current 15 Megawatts(MW)to 21 MW each, enabling them to achieve a higher output with less steam. These points were highly evaluated by KenGen and led to the adoption of the contract.

Kenya’s economic growth is spurring demand for power. The government has responded with a comprehensive blueprint for development, Vision 2030, which currently includes provision for boosting Kenya’s electricity generating capacity from renewable sources and seeking to transition to 100% green energy by 2030. Many new geothermal power plants are planned to tap into the 9GW geothermal potential in Kenya’s Great Rift Valley region.

Sunday 21 April 2024

DKT. NCHEMBA ATETA NA UONGOZI WA USAID

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) ukiongozwa na Msaidizi wa Utawala anayesimamia Afrika, Dkt. Monde Muyangwa, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Tanzania. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Washington D.C, nchini Marekani na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru na Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA, Bw. Mcha Hassan Mcha.

Ushirikiano wa Tanzania na Marekani umetimiza zaidi ya miaka 50 ambapo makubaliano ya kwanza ya kuanzishwa kwa uhusiano huo yalisainiwa mwaka 1968.


Friday 19 April 2024

NMB PESA AKAUNTI YAWAVUTIA WAKAGUZI WA NDANI AFRIKA, ARUSHA

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Happiness Laizer pembezoni mwa Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Katikati ni Meneja Mahusiano Huduma za Serikali wa NMB Kanda ya Kaskazini, Peter Masawe.

Ubunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na uwekezaji wenye tija inaoufanya kuwahudumia wateja kwa ufanisi vimekuwa kivutio kikubwa kwenye mkutano wa wakaguzi wa ndani wa Afrika unaofikia tamati leo jijini Arusha.


Wafanyakazi kwenye banda la benki hiyo katika viwanja vya Ukumbi wa AICC unapofanyika mkutano huo wamesema moja ya vitu vinavyowavutia wajumbe wanaowatembelea ni bidhaa ya NMB Pesa Akaunti kutokana na hasa urahisi na wepesi wa kuifungua.


NMB inatumia huduma hiyo, ambayo ni moja ya mikakati ya kufungua akaunti mpya za wateja milioni 1.5 mwaka huu, kutekeleza ajenda yake ya kuwajumuisha Watanzania zaidi kifedha na kupeleka huduma zake vijijini.


Aidha maafisa wa NMB walisema wajumbe wanaotembelea banda lao wanavutiwa pia na gharama nafuu ya TZS 1,000 ya kuifungua akaunti ya NMB Pesa pamoja na uwezo wake wa kumwezesha inayehimiliki kukopa hadi TZS 500,000 kwa kutumia simu ya mkononi kupitia huduma ya Mshiko Fasta.


Kwa mujibu wa Meneja wa tawi la NMB Clock Tower Arusha, Bw Praygod Mphuru, benki hiyo ni moja ya wadhamini wa mkutano huo wa siku tatu uliofunguliwa rasmi Jumatano na Makamu wa Rais, Dr Philip Mpango.


Mkutano huo ulitanguliwa na kikao maalumu cha siku mbili ambacho nacho maafisa waandamizi wa NMB walishiriki kikamilifu kwa ajili ya kubalishana uzoefu, kujifunza vitu vipya na kwenda sambamba na mabadiliko yanayotokea katika tasnia ya usimamizi wa ndani duniani.

Mikutano hiyo miwili imeudhuriwa na takribani wajumbe 2000 wengi wakiwa Watanzania na wengine wakitoka katika nchi 26 za Afrika pamoja na mataifa kadhaa nje ya bara hili.

“Tunautumia pia mkutano huu kwa ukubwa wake kama fursa ya kuonyesha umahili wetu wa kutoa huduma bora, ubunifu mkubwa wa bidhaa na jinsi tunavyowekeza vilivyo katika teknolojia mpya za kisasa,” Bw Mphuru alibainisha.

DKT. NCHEMBA: TANZANIA IMEPIGA HATUA KIUCHUMI NA KIDEMOKRASIA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa nne kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Alice Albright (wa tano kulia), Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden (wa tano kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tatu kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dkt. Juma Malik Akil (wa nne kushoto), Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru (wa kwanza kulia), Mratibu wa Tanzania wa Mradi wa MCC Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa pili kulia), Kiongozi wa Timu ya MCC nchini Tanzania Bw. Nilan Fernando (kushoto), Kamishna wa Idara Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade na Makamu wa Rais wa MCC anayeshughulikia Sera na ukaguzi, Bi. Alicia Mandaville, mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wao uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Washington D.C, ambapo walijadiliana ushirikiano wa shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga katika mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea nchini Marekani.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Alice Albright, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Washington D.C, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). inayoendelea nchini Marekani, ambapo walijadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kufanya mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), akiagana na Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden, baada ya kumalizika kwa Mkutano wao uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Washington DC.
Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), ukiwa katika mkutano na Uongozi wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), ambapo walijadiliana masuala ya ushirikiano Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs).
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) na Uongozi wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC).
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani) na Uongozi wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC).
Uongozi wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), ukifuatilia kwa umakini majadiliano kati yake na Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), katika Mkutano wao uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Washington D.C.
Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Uongozi wa Shirika hilo na Ujumbe wa Tanzania.

Na Benny Mwaipaja, Washington D.C.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amelihakikishia Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation-MCC) kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala ya haki za binadamu, utawala bora, demokrasia na usimamizi imara wa uchumi wa nchi.

Dkt. Nchemba amesema hayo alipoongoza ujumbe wa Tanzania, kukutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Shirika hilo, ukiongozwa na Makamu wake wa Rais Mhe. Alicia Mandaville, Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pande hizo mbili zilijadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa mpango wa kusaidia mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kutatua vikwazo vya ukuaji uchumi, kupitia ruzuku itakayotolewa na Shirika hilo.

Alisema kuwa hatua hiyo si tu kwamba ni utekelezaji wa vigezo vilivyowekwa na Shirika hilo ili Tanzania iweze kunufaika na mpango huo unaolenga kutoa misaada ya kiufundi, bali ni nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kulinda uhuru wa watu.

Dkt. Nchemba aliihakikishia MCC kwamba Tanzania iko tayari kushirikiana na Serikali ya Marekani katika mpango huo na kuuomba uongozi huo kuuamini mchakato huo na ikiwezekana kuipatia nchi mradi mkubwa wa COMPACT II, utakao iwezesha nchi kupata fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati katika sekta za usafirishaji, nishati, na maji.

EXCITING CAREER OPPORTUNITIES AT NMB BANK PLC


We are a leading bank, committed to your growth and welfare. Join our team of best talents in the market, together we will continue to impact and transform lives through meaningful work, innovative products and solutions while driving the sustainability agenda. 

We are renowned for investing, nurturing and transforming careers. Our commitment to diversity, equity and inclusion has led us to become the first financial institution in Africa to attain the most coveted EDGE Certification (EDGE Assess). We are more than a bank.

The following vacancies are currently available;
  • Insights & Customer Journey Manager - Head Office (Closing date; 23 April 2024)
  • Relationship Manager; Mortgage Financing - Highlands Zone (Closing date; 30 April 2024)
  • Senior Audit Associate; Data Analytics - Head Office (Closing date; 22 April 2024)
  • Senior Manager; Affluent - Head Office (Closing date; 23 April 2024)
  • Senior Manager; Corporate Banking - Head Office (Closing date; 26 April 2024)
  • Senior Manager; Mass Liabilities - Head Office (Closing date; 26 April 2024)

IMPACT BUSINESS BREAKFAST, 24 APRIL 2024 - HYATT REGENCY DAR ES SALAAM


BERNICE FERNANDES APPOINTED AS BOARD MEMBER FOR GLOBAL ENTREPRENEURSHIP FESTIVAL


In a significant development, Bernice Fernandes, a prominent figure in Tanzania's entrepreneurial landscape, has been appointed as a Board Member for the esteemed Global Entrepreneurship Festival. The festival, renowned as the world's largest entrepreneurship event, is poised to attract over 20 million viewers globally, with 12 concurrent events scheduled to unfold.

Set against the backdrop of the Entrepreneurship Village (E-Village) in Ondo State, Nigeria—a burgeoning hub often likened to Africa's Silicon Valley—the festival promises a convergence of global business titans, political leaders, and aspiring entrepreneurs.



Under the esteemed patronage of Nigeria's President, His Excellency Bola Ahmed Tinubu, and the distinguished presence of Africa's wealthiest woman, Folorunso Alakija, the festival garners unprecedented momentum. Noteworthy luminaries such as the CEO of Reebok, the Director General of the World Trade Organization, and the President of the African Development Bank, among others, are slated to grace the event with their insights.

The festival's agenda is as diverse as it is compelling, featuring a plethora of activities ranging from startup pitch competitions to a women's congress, leadership forums, trade fairs, and innovation showcases. With elements like hackathons, fashion shows, and concerts, the festival promises a dynamic blend of business and cultural exchange.

At the helm of this global initiative stands Bernice Fernandes, Founder and CEO of the Accelerate Business Group and the Accelerate Women's Initiative in Tanzania. Armed with an impressive academic pedigree—including an MBA in Entrepreneurship, a Masters in International Business, and a Bachelors in Finance from the United States—Bernice is eminently qualified to serve on international boards.

Accelerate Business Group is a business advisory firm for growth, providing strategic consulting, corporate training, coaching as well as facilitation services.

Accelerate Women's Initiative hosts executive conferences, masterclasses as well as a powerful networking platform for women in business. 

VODACOM YAZINDUA SIMUJANJA MAALUMU KWA WATEJA WENYE ULEMAVU

Balozi wa Pakistani nchini, Siraj Ahmad Khan (kushoto), Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Digit, Abdul Rehman Mahmood (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa simu maalum iitwayo 'Smart Kitochi+' kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kuona na kusikia huku ikiongeza matumizi ya dijitali nchini. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam – Aprili 18, 2024: Ili kuimarisha ushirikishwaji na kuongeza matumizi ya huduma na bidhaa za kidijitali nchini, kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC imezindua simujanja ya kidijitali inayoitwa 'Smart Kitochi +' ambayo imeundwa ikiwa na vipengele muhimu kwa ajili ya wateja wasiosikia na wasioona.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Bi. Linda Riwa, amesema kuwa uzinduzi huu ni sehemu ya juhudi endelevu za kampuni hiyo za kukuza ushirikishwaji huku ikiunga mkono serikali katika azma yake ya kuchochea matumizi ya bidhaa na huduma za kidigitali.


"Tunafurahia mapinduzi haya ya kuleta bidhaa na huduma za kidigitali na za kibunifu kwa wateja wetu wenye mahitaji mbalimbali kote nchini. Leo, tunazindua simu ya kipekee ya kidijitali inayoitwa 'Smart Kitochi+' ambayo mbali na sifa kama kioo kikubwa na cha kugusa, uwezo mkubwa wa kuhifadhi na betri inayodumu muda mrefu, simu hii pia itawanufaisha wateja wetu wenye ulemavu wa kusikia na kuona,” anasema Linda.


“Simu hii inajumuisha teknolojia ya kugusa na sauti, ikiruhusu wateja wenye changamoto hizi kupata huduma zetu bila kutegemea msaada wa mtu mwingine. Haya ni mapinduzi muhimu katika sekta ya utoaji huduma za mawasiliano, ikizingatiwa kuwa serikali inahimiza watoa huduma kuzingatia ushirikishwaji katika utoaji wa huduma kwa wateja,” aliongeza Linda.


Uzinduzi wa simu hii ni ingizo la kipekee sokoni ukilinganisha na matoleo mengine, ikiwa na uwezo wa kuchochea ushirikishwaji katika matumizi ya huduma za mawasiliano ya kidigitali. Pia ina ubora wa hali ya juu ikiwa na kioo kikubwa na cha kugusa (2.8”), uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu kwenye 8GB na betri inayodumu muda mrefu ya 3000mAh.

Toleo hili jipya la 'Smart Kitochi+' ni sehemu ya juhudi za Vodacom kuwapeleka wateja wake kwenye matumizi ya kidigitali, ikiwa ni pamoja na mtandao wa 4G, ambao bado una watumiaji wachache ikilinganishwa na idadi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini Tanzania.

"Tunajivunia kuwa mtandao unaoongoza nchini, tukitoa huduma za kidigitali za ubunifu kwa zaidi ya wateja milioni 21. Kuwa na idadi kubwa ya wateja pekee haitoshi; tunataka wateja wetu wanufaike na mapinduzi ya kidigitali yanayoendelea na ubunifu mkubwa tunaoingiza kwenye bidhaa zetu. Kwa kuanzisha bidhaa za kisasa kama 'Smart Kitochi+' tunaamini tutachochea wateja wengi zaidi kuhama kutoka kwenye mfumo wa 2G na kuanza kufurahia huduma mbalimbali za kidigitali zinazotolewa na mtandao wetu wa kasi wa 4G na 5G uliosambaa nchini na hatimaye kuongeza matumizi ya simujanja ambayo kwa sasa ni asilimia 32," alifafanua Bi. Linda.

Thursday 18 April 2024

FA CUP SEMI-FINALS MAN CITY vs CHELSEA NDANI YA DStv COMPACT

 

TIGO YAZINDUA FIBER KWA AJILI YA INTANETI YA NYUMBANI NA OFISINI

Mkuu wa Kitengo cha Tigo Biashara, John Sicilima akiwaelezea waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma mpya ya Tigo Fiber kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na maofisini. Kulia ni Mkuu wa Chapa na Mawasaliano Tigo, Anna Loya.
  • Mji wa Mbweni jijini Dar es Salaam kuwa mnufaika wa kwanza wa huduma hii ya intaneti
Dar es Salaam, Aprili 16, 2024: Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali nchini Tanzania, Tigo, imezindua huduma ya mtandao ya kwanza ya aina yake ya Fiber to Home na Fiber to Office ambayo imeundwa kuwezesha watumiaji na wafanyabiashara kupata huduma za uhakika, na intaneti yenye spidi nyumbani na Ofisini.

Huduma hii muhimu inasisitiza dhamira ya Tigo ya kusaidia mabadiliko ya kidijitali nchini Tanzania kwa kusambaza teknolojia na huduma za kisasa zinazomnufaisha kila mtumiaji nyumbani na maeneo ya biashara.

Akizungumzia dhamira ya Tigo ya kuleta mabadiliko katika hali ya kidijitali nchini Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania, Kamal Okba alisema, “Tunajivunia kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano kuzindua mtandao wa Fiber hadi Nyumbani na Ofisini nchini Tanzania. Hii inaimarisha nafasi yetu kama viongozi katika mageuzi ya mtindo wa maisha ya kidijitali na wakati huo huo ikichangia katika utekelezaji wa ajenda ya kidijitali ya Tanzania.”

Naye Mkuu wa Chapa (Brand) na Mawasiliano Tigo, Anna Loya, alisema, “Tuna dhamira ya ubunifu na kuridhika kwa wateja, tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika kusambaza teknolojia ya kisasa ya fiber ili kutoa uzoefu usio na kifani wa muunganisho. kuwezesha biashara na kaya na tija na ushirikiano ulioimarishwa. Huduma mpya ya Tigo Fiber inaahidi kasi ya mtandao ya kasi zaidi, huduma zisizo na kifani na usaidizi kwa wateja ili kuleta mapinduzi katika namna Watanzania wanavyoungana na kujihusisha na ulimwengu wa kidijitali.”

DKT. NCHEMBA ATETA NA UONGOZI WA IMF KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (The Executive Director of the IMF– Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Willie Nakunyada (wapili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa pili kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (wa kwanza kushoto), na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yenye kauli mbiu ya “Vision to Impact” inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani. Katika kikao hicho tathmini ya mwenendo wa uchumi wa Tanzania ilijadiliwa pamoja na utekelezaji wa program ya IMF chini ya mpango wa "Extended Credit Facility-(ECF)" inayofanikisha utekelezaji wa Sera za kiuchumi na upatikanaji wa mikopo nafuu kwa nchi kutoka kwa washirika wa maendeleo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (The Executive Director of the IMF– Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Willie Nakunyada, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (The Executive Director of the IMF– Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Willie Nakunyada, akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), aliyeongoza ujumbe wa Tanzania, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akisikiza jambo wakati wa kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (The Executive Director of the IMF– Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Willie Nakunyada. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (kushoto).
Ujumbe wa Tanzania (kulia) ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wanne kulia), ukiwa katika kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (The Executive Director of the IMF– Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Willie Nakunyada, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yenye kauli mbiu ya “Vision to Impact” inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tatu kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (wa tano kulia), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (wapili kulia) na Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade (wa sita kulia).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika la Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (The Executive Director of the IMF– Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Willie Nakunyada.

Na Benny Mwaipaja, Washington D.C.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameliambia Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwamba utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali unaathiriwa na hali mbaya ya hewa inayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi ambapo kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingeelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi kinaelekezwa kukabiliana na athari za mafuriko yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania kufuatia mvua za el nino zinazoendelea kunyesha.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipoongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Willie Nakunyada, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Alisema kuwa wakati wa utekelezaji wa Bajeti inayoendelea ya mwaka 2023/2024 mabadiliko ya tabianchi yameathiri mtiririko wa utoaji wa fedha kwenda kwenye miradi ambayo ingesaidia kwa kiasi kikubwa kuchachua shughuli za kiuchumi badala yake zinatumika kurekebisha miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko ikiwemo madaraja, barabara, na miundombinu mingine ya huduma za jamii.